Swahili

Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Kwenye kipindi kile ambacho Petro alikuwa na Yesu, aliona sifa nyingi za kupendeza ndani ya Yesu, hali nyingi zenye za kustahili kuigwa, na nyingi ambazo zilizomkimu. Ingawa Petro aliona nafsi ya Mungu ndani ya Yesu katika njia nyingi, na kuona sifa nyingi za kupendeza, mara ya kwanza hakumjua Yesu. Petro alianza kumfuata Yesu alipokuwa na umri wa miaka 20, na akaendelea kufanya hivyo kwa miaka sita. Kwenye kipindi hiki cha muda, hakuwahi kupata kumjua Yesu, lakini alikuwa radhi kumfuata Yeye kutokana tu na kuvutiwa na Yeye. Wakati Yesu alipomwita kwanza kwenye ufuko wa Bahari ya Galilaya, Aliuliza: “Simioni, mtoto wa Yona, je, utanifuata?” Petro akasema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu. Nitakufuata.” Wakati huo, Petro alikuwa amesikia kuhusu mwanamume mmoja aliyeitwa Yesu, nabii mkubwa zaidi kuliko wote, Mtoto mpendwa wa Mungu, na Petro alikuwa akitumai kila wakati kumpata, akitumai kupata fursa ya kumwona Yeye (kwa sababu hivyo ndivyo alivyoongozwa wakati huo na Roho Mtakatifu). Ingawa alikuwa hajawahi kumwona Yeye na alikuwa amesikia tu uvumi kuhusu Yeye, kwa utaratibu tamanio na kivutio cha kumwabudu Yesu vyote vikaongezeka katika moyo wake, na mara nyingi alitamani siku ile atakayomtazamia Yesu. Na Yesu alimwitaje Petro? Yeye pia alikuwa amesikia habari za mwanamume aliyeitwa Petro, na si kwamba Roho Mtakatifu alimwagiza: “Nenda katika Bahari ya Galilaya, pale ambapo kunaye bwana mmoja anayeitwa Simioni, mtoto wa Yona.” Yesu alimsikia mtu akisema kwamba kulikuwa na bwana mmoja aliyeitwa Simioni, mtoto wa Yona, na kwamba watu walikuwa wamesikia mahubiri yake, kwamba yeye pia alihubiri injili ya ufalme wa mbinguni, na kwamba watu waliomsikiliza waliguswa kiasi cha wote kutokwa na machozi. Baada ya kusikia haya, Yesu alimfuata mtu huyu, na kuelekea kwenye Bahari ya Galilaya; wakati Petro alipoukubali mwito wa Yesu, alimfuata.

Kwenye kipindi hiki akimfuata Yesu, alikuwa na maoni mengi kuhusu Yeye na siku zote Alimhukumu kutokana na mtazamo wake. Ingawa alikuwa na kiwango fulani cha uelewa wa Roho Mtakatifu, Petro hakuwa ametiwa nuru sana, na haya yanaonekana kwenye maneno yake aliposema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu.” Hakuelewa mambo yale ambayo Yesu alifanya na wala hakupata nuru yoyote. Baada ya kumfuata kwa muda fulani alivutiwa na kile alichofanya Yeye na kusema, na kwa Yesu Mwenyewe. Alikuja kuhisi kwamba Yesu alivutia upendo na heshima; alipenda kujihusisha na Yeye na kuwa kando Yake, na kusikiliza maneno yake Yesu kulimpa ruzuku na msaada. Kwenye kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata uelewa wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichofanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. Aliona kwamba ingawa Yesu hakuwa na kimo kikubwa wala ubinadamu usio wa kawaida, Alikuwa na umbo la ajabu na lisilo la kawaida kwa kweli. Ingawa Petro hakuweza kuyafafanua kabisa, aliweza kuona kwamba Yesu alikuwa na mwenendo tofauti na kila mtu mwingine, kwani Aliyafanya mambo yaliyokuwa tofauti kabisa na yale yaliyofanywa na binadamu wa kawaida. Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi cha kwamba aligeuka na kuwa mwepesi na mchangamfu kama njiwa, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyeathirika na hali ya hewa. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayeguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na ukali vyote vikamfanya kuja kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.

Petro alikuwa ni binadamu mwenye akili, aliyekuwa na akili za kuzaliwa, ilhali aliyafanya mambo mengi ya kijinga alipokuwa akimfuata Yesu. Mwanzoni kabisa, alikuwa na fikira fulani kuhusu Yesu. Aliuliza: “Watu wanasema kuwa Wewe ni nabii, kwa hiyo ulipokuwa na umri wa miaka minane na mkomavu vya kutosha kutambua mambo, je ulijua kuwa wewe ni Mungu? Je ulijua kwamba mimba Yako ilitungwa na Roho Mtakatifu?” Yesu alijibu: “La, Sikujua! Kwani Sionekani kama mtu wa kawaida tu kwako? Mimi niko sawa na mtu yeyote mwingine yule. Yule mtu Baba hutuma ni mtu wa kawaida, na wala si mtu asiyekuwa wa kawaida. Na Ingawa kazi Ninayofanya inawakilisha Baba Yangu wa mbinguni, taswira Yangu, hulka Yangu na mwili Wangu haviwezi kuwakilisha kikamilifu Baba Yangu wa mbinguni, ni sehemu moja tu Yake. Ingawa Nilitoka kwenye Roho, mimi Ningali mtu wa kawaida, naye Baba Yangu alinituma mimi hapa ulimwenguni kama mtu wa kawaida, wala si mtu asiyekuwa wa kawaida.” Ni wakati tu Petro aliposikia haya ndipo alipopata uelewa kidogo kuhusu Yesu. Na ilikuwa tu baada ya kupitia saa nyingi zisizohesabika za kazi ya Yesu, mafunzo Yake, uchungaji Wake, na uendelevu Wake, ndipo alipopata uelewa wa kina zaidi. Katika mwaka Wake wa 30, Yesu alimwambia Petro kuhusu kusulubishwa Kwake kujako, kwamba Alikuwa amekuja kufanya kazi ya kusulubishwa ili kukomboa wanadamu wote. Alimwambia pia kwamba siku tatu baada ya kusulubishwa Kwake, mwanadamu angefufuka tena, na baada ya kufufuka angeonekana kwa watu kwa siku 40. Petro alikuwa na huzuni baada ya kusikia maneno haya, lakini akawa karibu zaidi na Yesu huku akiathiriwa na maneno Yake. Baada ya kushuhudia mambo haya kwa muda fulani, Petro alikuja kutambua kwamba kila kitu Yesu alichofanya kilitokana na nafsi ya Mungu, na akaja kufikiria kwamba Yesu alikuwa wa kupendeka ajabu. Pale tu alipokuja kuwa na uelewa huu ndipo Roho Mtakatifu alimtia nuru kutoka ndani yake. Kisha Yesu akawageukia wanafunzi wake na wafuasi wengine na kusema: “Yohana, wewe unasema Mimi ni nani?” Yohana akajibu: Wewe ni Musa.” Kisha akamgeukia Luka: “Na wewe, Luka, wewe unasema Mimi ni nani?” Luka akajibu: “Wewe ndiwe mkubwa zaidi kati ya manabii.” Kisha akamwuliza mtawa: “Wewe nawe unasema Mimi ni nani?” Mtawa akajibu: “Wewe ndiwe nabii mkubwa zaidi anayeongea maneno mengi kutoka milele hadi milele. Hakuna unabii wa yeyote yule mwingine ambao ni mkubwa kama Wako, wala hekima ya yeyote yule mwingine kubwa kama Yako; Wewe ni nabii.” Kisha Yesu akamgeukia Petro na kusema: “Petro, wewe nawe unasema Mimi ni nani” Petro akajibu: “Wewe ndiwe Kristo, Mtoto wa Mungu Aliye hai. Unatoka mbinguni, Wewe si wa ulimwenguni, Wewe si sawa na viumbe vya Mungu. Sisi tuko ulimwenguni na Wewe u pamoja nasi hapa, lakini Wewe ni wa mbinguni, Wewe si wa ulimwengu, na Wewe si wa ulimwengu.” Ni kupitia katika hali hii ndipo Roho Mtakatifu alipomtia nuru, hali iliyomwezesha kuwa na uelewa huu. Baada ya kutiwa nuru huku, alivutiwa na kila kitu ambacho Yesu alikuwa amefanya hata zaidi, alimfikiria Yeye kuwa mwenye upendo zaidi, na siku zote alikuwa moyoni mwake asitake kutengana na Yesu. Kwa hiyo, mara ya kwanza Yesu alipojifichua kwake Petro baada ya kusulubishwa na kufufuka Petro alilia kwa furaha ya kipekee: “Bwana! Umefufuka!” Kisha, huku akilia, alimvua samaki mkubwa ajabu, akampika na kumpakulia Yesu. Yesu alitabasamu, lakini hakuongea. Ingawa Petro alijua Yesu alikuwa amefufuka, hakuelewa fumbo hilo. Alipompa Yesu samaki yule kumla, Yesu hakukataa na ilhali hakuongea wala kuketi chini kula, lakini badala yake alitoweka ghafla. Huu ulikuwa ni mshtuko wa ajabu kwake Petro, na hapo tu ndipo alipoelewa ya kwamba yule Yesu aliyefufuka alikuwa tofauti na yule Yesu wa awali. Baada ya kutambua hili, Petro alihuzunika, lakini pia akapata tulizo kwa kujua kwamba Bwana alikuwa amekamilisha kazi Yake. Alijua kwamba Yesu alikuwa amekamilisha kazi Yake, kwamba muda Wake wa kukaa na binadamu ulikuwa umeisha, na kwamba binadamu angelazimika kutembea kwa njia yake kuanzia hapo. Yesu aliwahi kumwambia: “Lazima pia unywe kutoka kwenye kikombe kikali nilichonywea Mimi (hili ndilo alilomwambia baada ya kufufuka), lazima utembee njia niliyotembea Mimi, lazima uyapoteze maisha yako kwa ajili Yangu.” Tofauti na sasa, kazi wakati huo haikuchukua mfumo wa mazungumzo ya uso kwa uso. Kwenye Enzi ya Neema, kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa fiche sana, naye Petro aliteseka kupitia kwa ugumu mwingi, na wakati mwingine angefikia kiwango cha kumaka: “Mungu! Sina chochote ila maisha haya. Ingawa hayana thamani Kwako, ningependa kuyatoa Kwako. Ingawa binadamu hawastahili kukupenda, na upendo wao na mioyo yao haina thamani, naamini kwamba unaweza kuona nia iliyomo kwenye mioyo ya binadamu. Na hata Ingawa miili ya binadamu haifikii ukubalifu Wako, ningependa Wewe uweze kuukubali moyo wangu.” Baada ya kutamka maombi haya angepata himizo, haswa wakati alipoomba: “Nitautoa moyo wangu wote kwa Mungu. Ingawa siwezi kumfanyia Mungu chochote, nitamtosheleza Mungu kwa utiifu na kujitolea Kwake kwa moyo wangu wote. Ninaamini Mungu lazima auangalie moyo wangu.” Alisema: “Siombi chochote katika maisha yangu ila fikira zangu za upendo kwa Mungu na tamanio la moyo wangu kuweza kukubaliwa na Mungu. Nilikuwa naye Bwana Yesu kwa muda mrefu, ilhali sikuwahi kumpenda Yeye, hili ndilo deni langu kubwa zaidi. Ingawa niliishi na Yeye, sikumjua, na hata niliweza kuzungumza maneno yasiyofaa kama hayupo. Kufikiria kuhusu mambo haya kunanifanya kuhisi ni kana kwamba napaswa kumshukuru zaidi Bwana Yesu.” Siku zote aliomba kwa njia hii. Alisema: “Mimi sifai zaidi ya vumbi. Siwezi kufanya chochote ila nautoa moyo huu mtiifu kwa Mungu.”

Kulikuwepo na kilele katika yale yote Petro alipitia, wakati mwili wake ulinyenyekea zaidi, lakini Yesu akampa himizo ndani kwa ndani. Na akajitokeza kwake mara moja. Wakati Petro alikuwa katika mateso makuu na moyo wake ulikuwa taabani, Yesu alimwelekeza: “Ulikuwa na Mimi ulimwenguni, na Nilikuwa na wewe hapa. Na Ingawa awali tulikuwa pamoja mbinguni, kwa hakika, huko ni, ulimwenguni kwa kiroho. Sasa Nimerudi kwenye ulimwengu wa kiroho, na wewe umo ulimwenguni. Kwani Mimi si wa ulimwengu, na Ingawa wewe pia si wa ulimwengu, lazima utimize kazi yako hapa ulimwenguni. Kwani wewe ni mtumishi, lazima uwajibike kwa njia bora zaidi uwezayo.” Petro alipata tulizo, kwa kusikia kwamba angeweza kurudi kwa upande wa Mungu. Wakati Petro alipokuwa katika masumbuko hayo karibu hali yake iwe mahututi kitandani, alisikitika kiasi cha kusema hivi: “Nimepotoka kwelikweli, siwezi kumtosheleza Mungu.” Yesu alijitokeza kwake na kusema: “Petro, huenda ikawa umesahau azimio ulilowahi kunitamkia Mimi? Je, kwa kweli umesahau kila kitu Nilichosema? Umesahau azimio ulilonitajia?” Petro aliona kwamba alikuwa Yesu na akainuka kutoka kitandani, naye Yesu akamkabili na kusema: “Mimi si wa ulimwengu, tayari Nimekuambia wewe—hili lazima uelewe, lakini umesahau kitu kingine Nilichokuambia? ‘Wewe pia si wa ulimwengu, si wa dunia.’ Sasa hivi kunayo kazi unayohitaji kufanya, huwezi kuhuzunika namna hivi, huwezi kuteseka hivi. Ingawa binadamu na Mungu hawawezi kuishi pamoja kwenye ulimwengu mmoja, Ninayo kazi Yangu na wewe unayo yako, na siku moja wakati kazi yako imekamilika, tutakuwa pamoja katika himaya moja, nami Nitakuongoza wewe kuwa pamoja Nami milele na milele.” Petro alipata tulizo na hakikisho baada ya kuyasikia maneno hayo. Alijua kuteseka huku kulikuwa ni jambo ambalo lazima angevumilia na kupitia, na akapata mhemko kuanzia hapo. Yesu alijitokeza haswa kwake katika ule muda muhimu, akimpa fahamisho na mwongozo maalum, na akifanya kazi nyingi ndani yake. Na ni nini ambacho Petro alijutia zaidi? Yesu alimwuliza Petro swali jingine (Ingawa haijarekodiwa kwenye Biblia kwa njia hii) si kipindi kirefu baadaye Petro alikuwa amesema “Wewe ndiwe Mtoto wa Mungu aliye hai,” nalo swali lenyewe lilikuwa: “Petro! Umewahi kunipenda?” Petro alielewa kile alichomaanisha, na kusema: “Bwana! Niliwahi kumpenda Baba wa mbinguni, lakini nakubali sijawahi kukupenda Wewe.” Yesu naye akasema: “Kama watu hawampendi Baba wa mbinguni, watawezaje kumpenda Mtoto hapa ulimwenguni? Na kama watu hawampendi Mtoto aliyetumwa na Mungu, Baba, wanawezaje kumpenda Baba aliye mbinguni? Kama kweli watu wanampenda Mtoto aliye ulimwenguni, basi kwa kweli wanampenda Baba aliye mbinguni.” Wakati Petro alipoyasikia maneno haya aligundua upungufu wake. Siku zote alihisi huzuni hadi kiwango cha kulengwalengwa na machozi machoni kutokana na maneno yake “niliwahi kumpenda Baba wa mbinguni, lakini sikuwahi kukupenda Wewe.” Baada ya ufufuo na kupaa angani kwa Yesu alihuzunika na kuwa na simanzi zaidi kwa yale yote yaliyokuwa yamefanyika. Huku akikumbuka kazi yake iliyopita na kimo chake cha sasa, mara nyingi angekuja mbele ya Yesu kwa maombi, siku zote akiwa na hisia za majuto na masikitiko kwa kutoweza kutosheleza tamanio la Mungu, na kutoweza kufikia viwango vya Mungu. Masuala haya yakawa ndiyo mzigo wake mkubwa. Alisema: “Siku moja nitatoa kila kitu changu nilichonacho na kila kitu kinachonifanya mimi kuwa mimi kwa ajili Yako, nitakupa kile chenye thamani zaidi.” Alisema: “Mungu! Ninayo imani moja tu na upendo mmoja tu. Maisha yangu hayana thamani ya chochote, na mwili wangu hauna thamani ya chochote. Ninayo imani moja tu na upendo mmoja tu. Ninayo imani kwako Wewe katika akili yangu na upendo Kwako wewe katika moyo wangu; mambo haya mawili tu ndiyo niliyonayo kukupatia Wewe, na wala sina kingine chochote.” Petro alihimizwa pakubwa na maneno yake Yesu, kwa sababu kabla ya Yesu kusulubishwa alikuwa amemwambia: “Mimi si wa ulimwengu huu, na wewe pia si wa ulimwengu huu.” Baadaye, wakati Petro alipofikia hali ya maumivu makali, Yesu alimkumbusha: “Petro, je, umesahau? Mimi si wa ulimwengu huu, na ni kwa ajili tu ya kazi Yangu ndipo Niliondoka mapema. Wewe pia si wa ulimwengu huu, umesahau? Nimekuambia mara mbili, kwani hukumbuki?” Petro alimsikia na kumwambia: “Sijasahau!” Yesu naye akasema: “Uliwahi kuwa na wakati mzuri ukiwa umekusanyika pamoja na Mimi kule mbinguni na kwa kipindi fulani kando Yangu mimi. Unanidata Mimi, na Mimi ninakudata. Ingawa viumbe hivi havistahili kutajwa katika macho Yangu, ninawezaje kukosa kupenda yule ambaye hana hatia na anapendeka? Je, umesahau ahadi Yangu? Lazima ulikubali agizo Langu hapa ulimwenguni, lazima utimize kazi Niliyokuaminia. Bila shaka siku moja Nitakuongoza kuwa kando Yangu.” Baada ya kuyasikia haya, Petro akahimizwa zaidi, na kupata mhemko mkubwa zaidi, kiasi cha kwamba alipokuwa msalabani, aliweza kusema hivi: “Mungu! Siwezi kukupenda vya kutosha! Hata ukiniomba kufa, siwezi bado kukupenda vya kutosha! Popote Utakapotuma nafsi yangu, utimize au ukose kutimiza ahadi Zako, chochote ufanyacho baadaye, ninakupenda na ninakuamini.” Kile alichoshikilia kilikuwa imani yake, na upendo wa kweli.

Jioni moja, wanafunzi mbalimbali, akiwemo Petro, walikuwa kwenye mashua ya kuvulia samaki. Walikuwa pamoja naye Yesu, naye Petro akamwuliza Yesu swali la kijinga sana: “Bwana! kunalo swali ambalo nimekuwa nalo kwa muda mrefu sana ambalo ningependa kukuuliza Wewe.” Yesu alijibu: “Yesu akajibu basi uliza tafadhali!” Petro naye akauliza: “Je, kazi iliyofanywa kwenye Enzi ya Sheria ilitokana na Wewe?” Yesu akatabasamu, kana kwamba alikuwa akisema: “Mtoto huyu, unawezaje kuuliza swali la kijinga hivyo!” Kisha akaendelea kwa kusudio: “Haikuwa kazi Yangu hiyo, ilikuwa kazi ya Yehova na Musa.” Petro akasikia haya na kushangaa: “Salaale! Kwa hivyo haikuwa kazi Yako.” Punde tu Petro aliposema hayo, Yesu hakuongea tena. Petro akajifikiria kimyakimya: “Si Wewe uliofanya kazi hiyo, kwa hiyo ndiyo maana umekuja kuiangamiza sheria, kwani hiyo haikuwa kazi Yako.” Moyo wake ukapata “tulizo” pia. Baadaye, Yesu akatambua kwamba Petro alikuwa mjinga kiasi, lakini kwa sababu hakuwa na utambuzi wowote wakati huo, Yesu hakusema chochote kingine au kumkemea waziwazi. Siku moja Yesu alihubiri kwenye sinagogi, na watu wengi walikuwepo, akiwemo Petro, ili aweze kumsikiliza akihubiri. Yesu akasema: “Yule atakayekuja kutoka milele hadi milele atafanya kazi ya ukombozi kwenye Enzi ya Neema, kuwakomboa wanadamu wote kutoka kwa dhambi, lakini, hatazuiliwa na taratibu zozote katika kumwongoza binadamu nje ya dhambi. Atatembea kutoka kwenye sheria na kuingia kwenye Enzi ya Neema. Atakomboa wanadamu wote. Atapiga hatua mbele kutoka kwenye Enzi ya Sheria hadi kwenye ile Enzi ya Neema, ilhali hakuna atakayemjua Yeye, Yule aliyekuja kutoka kwa Yehova. Kazi aliyofanya Musa hakupewa na Yehova; Musa aliziandika sheria kwa sababu ya ile kazi ambayo Yehova alikuwa amefanya.” Baada ya kusema, aliendelea: “Wale watakaotupilia mbali mafundisho ya Enzi ya Neema kwenye Enzi ya Neema watakumbana na janga. Lazima wasimame kwenye hekalu na kupokea maangamizo ya Mungu, nao moto utakuwa juu yao.” Baada ya Petro kumaliza kusikiliza haya, alikuwa na mwitikio wa aina fulani katika hayo aliyoyasikia. Kwenye kipindi cha kile alichopitia, Yesu alichunga na kumtunza Petro, huku akiongea naye mazungumzo ya moyo kwa moyo, jambo ambalo lilimpatia Petro uelewa bora zaidi kiasi kuhusu Yesu. Wakati Petro alipofikiria kuhusu mahubiri ya Yesu ya siku hiyo, kisha swali alilowahi kumwuliza Yesu walipokuwa kwenye mashua ya kuvua samaki nalo jibu alilopewa na Yesu, pamoja na vile alipocheka, ndipo alipoelewa kila kitu. Baadaye, Roho Mtakatifu alimtia nuru Petro, na kupitia kwa haya tu ndipo alipoelewa kwamba Yesu alikuwa Mtoto wa Mungu aliye hai. Uelewa wa Petro ulitokana na kutiwa nuru na Roho Mtakatifu, lakini kulikuwepo na mchakato katika uelewa huu. Ilikuwa kupitia kwa kuuliza maswali, kusikiliza mahubiri ya Yesu, kisha kupitia kupokea ushirika maalum wa Yesu na uchungaji Wake maalum, ndipo Petro alipokuja kutambua Yesu kuwa Mtoto wa Mungu Aliye hai. Haya yote hayakufikiwa usiku kucha; ulikuwa ni mchakato, na huu ukawa ni msaada kwake katika yale yote aliyopitia baadaye. Kwa nini Yesu hakufanya kazi ya kufanya kuwa timilifu kwa watu wengine, lakini Petro tu? Kwa sababu Petro tu ndiye aliyeelewa kwamba Yesu ndiye aliyekuwa Mtoto wa Mungu aliye hai na hakuna mwingine aliyejua hili. Ingawa kulikuwa na wanafunzi wengi waliojua mengi wakati wao na waliomfuata Yeye, maarifa yao yalikuwa ya juujuu tu. Na ndiyo maana Petro alichaguliwa na Yesu kuwa mfano wa kufanywa kuwa timilifu. Kile Yesu alichomwambia Petro wakati huo ndicho anachowaambia watu leo, ambao maarifa na maonyesho yao ya maisha lazima yafikie yale ya Petro. Ni kulingana na mahitaji haya na njia hii ndipo Mungu atakapofanya kila mtu kuwa timilifu. Kwa nini watu leo wanahitajika kuwa na imani halisi na upendo wa kweli? Kile Petro alichopitia pia nyinyi lazima mpitie, yale matunda Petro alifaidi kutoka kwenye yale yote aliyopitia pia lazima yaonyeshwe ndani yenu, na maumivu aliyoteseka Petro, nyinyi pia lazima mtayapitia kwa kweli. Njia mnayotembelea ndiyo ile ile ambayo Petro alitembelea. Maumivu mnayoteseka ndiyo maumivu ambayo Petro aliteseka. Mnapopokea utukufu na mnapoishi kwa kudhihirisha maisha halisi, basi mnaishi kwa kudhihirisha taswira ya Petro. Njia ni ileile, na kulingana na haya ndipo mtu anafanywa kuwa timilifu. Hata hivyo, marika ya watu wa leo kwa kiasi fulani yanao upungufu yakilinganishwa na yale ya Petro, kwani nyakati zimebadilika, na ndivyo pia hali ya kupotoka. Na pia kwa Yudea kulikuwepo ufalme wa kipindi kirefu uliokuwa na utamaduni wa kale. Kwa hiyo lazima mjaribu kuboresha marika yenu.

Petro alikuwa mtu mwenye akili razini, makini kwa kila kitu alichofanya, na pia mwaminifu kupindukia. Alikumbana na changamoto nyingi. Alikumbana na jamii akiwa na umri wa miaka 14, huku akihudhuria shule na mara nyingi akienda kwenye sinagogi. Alikuwa na shauku nyingi na siku zote alikuwa radhi kuhudhuria mikutano. Wakati huo, Yesu alikuwa hajaanza rasmi kazi Yake; huu ulikuwa ni mwanzo tu wa Enzi ya Neema. Petro alianza kukumbana na wahusika wa kidini alipokuwa na umri wa miaka 14; kufikia wakati alipokuwa na umri wa 18 alikumbana na wasomi wa kidini, lakini baada ya kushuhudia wasomi wa kidini uliokuwepo kila mahali, aliondoka. Na kwa kuona watu hao walivyokuwa wenye hila, wajanja, na waliojaa mabishano, aliudhika kabisa (hivi ndivyo Roho Mtakatifu alivyofanya kazi wakati huo, ili kumfanya kuwa timilifu. Roho Mtakatifu alimsukuma haswa na ikaweza kufanya kazi maalum ndani yake), na hivyo basi akaondoka kwenye sinagogi akiwa na umri wa miaka 18. Wazazi wake walimtesa na wasingemruhusu kuamini (walikuwa wa shetani, na hawakuwa na imani yoyote). Hatimaye, Petro alitoka nyumbani na kusafiri kwa mapenzi yake, huku akivua samaki na kuhubiri kwa miaka miwili, kipindi ambacho aliweza pia kuwaongoza watu wachache kiasi. Sasa unafaa uweze kuona waziwazi njia iliyochukuliwa na Petro. Kama umeiona waziwazi, basi huenda umejua kazi inayofanywa leo, kwa hiyo usingelalamika au kuwa mtulivu tu, au kutamani chochote. Unafaa kupitia hali halisi aliyopitia Petro wakati huo: Alikumbwa na huzuni; hakuomba tena kuwa na mustakabali wowote au baraka zozote. Hakutafuta faida, furaha, umaarufu, au utajiri wa ulimwengu na alitafuta tu kuishi maisha yenye maana zaidi, ambayo yalikuwa ya kulipiza upendo wa Mungu na kujitolea kile alichokuwa nacho cha thamani zaidi kwa Mungu. Kisha angetosheka katika moyo wake. Mara nyingi aliomba kwa Yesu akitumia maneno haya: “Bwana Yesu Kristo, niliwahi kukupenda Wewe, lakini sikukupenda Wewe kwa kweli. Ingawa nilisema nina imani kwako Wewe, sikuwahi kukupenda kwa moyo wa kweli. Nilikuwa nakutazamia tu, nikikuabudu Wewe, na kukupeza Wewe, lakini sikuwahi kukupenda Wewe au kuwa na imani ya kweli kwako Wewe.” Siku zote aliomba ili kutoa azimio lake, alihimizwa kila wakati na maneno yake Yesu[a] na kuyageuza kuwa motisha. Baadaye, baada ya kipindi cha kile alichopitia, Yesu alimjaribu yeye, akimchochea kumtaka Yeye zaidi. Alisema: “Bwana Yesu Kristo! Ninakupeza kweli, na kutamani kukutazamia. Ninakosa mengi mno, na siwezi kufidia upendo Wako. Ninakusihi kunichukua hivi karibuni. Utanihitaji mimi lini? Utanichukua lini? Ni lini nitakapoutazama uso Wako tena? Sitamani tena kuishi katika mwili huu, kuendelea kupotoka, na vilevile sipendi kuasi zaidi ya nilivyoasi. Niko tayari kujitolea kile nilichonacho Kwako wewe haraka iwezekanavyo, na singependa kukuhuzunisha Wewe zaidi ya hivi nilivyofanya.” Hivi ndivyo alivyoomba, lakini hakujua wakati huo kwamba Yesu angemfanya kuwa timilifu. Kwenye kipindi hicho cha makali ya majaribio yake, Yesu alijitokeza kwake tena na kusema: “Petro, Ningependa kukufanya kuwa timilifu, ili uwe kipande cha tunda ambacho kitaonyesha kugandishwa kwa wewe kufanywa kuwa timilifu na Mimi, ambacho Nitafurahia. Unaweza kweli kunishuhudia Mimi? Umefanya kile Nilichokuomba kufanya? Umeishi kwa kudhihirisha yale maneno Niliyoyaongea? Uliwahi kunipenda Mimi, lakini Ingawa ulinipenda Mimi, umezidi kwa kunipenda? Ni nini ulichonifanyia Mimi? Unatambua kwamba wewe hufai upendo Wangu, lakini wewe umenifanyia nini?” Petro aliona kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Yesu na akakumbuka kiapo cha awali cha kumpa Mungu maisha yake. Na kwa hiyo, hakulalamika tena, na maombi yake baadaye yakazidi kuwa bora zaidi. Akaomba, akisema: “Bwana Yesu Kristo! Niliwahi kukuacha Wewe, na Wewe pia uliwahi kuniacha mimi. Tumekuwa mbalimbali kwa kipindi cha muda, na muda kiasi tukiwa pia pamoja. Ilhali unanipenda mimi zaidi ya kila kitu kingine. Nimekuasi Wewe mara nyingi na nikakuhuzunisha mara nyingi. Ninawezaje kusahau mambo kama haya? Kazi uliyofanya ndani yangu mimi na kile kwenye akili yangu, huwa ulichoniaminia kwa imani ndicho ninachofikiria siku zote sisahau. Pamoja na kazi uliyonifanyia mimi nimejaribu kadri ya uwezo wangu. Unajua kile ninachoweza kufanya, na unajua zaidi wajibu ninaoweza kutekeleza. Ombi lako ndilo amri yangu na nitajitolea kila kitu nilichonacho Kwako. Wewe tu ndiwe unayejua kile ninachoweza kukufanyia Wewe. Ingawa Shetani alinidanganya sana na nikakuasi Wewe, ninaamini kwamba hunikumbuki mimi kwa dhambi hizo, kwamba hunichukulii mimi kutokana na hizo dhambi. Ningependa kuyatoa maisha yangu yote kwa ajili Yako wewe. Siombi chochote, na wala sina matumaini au mipango mingine; ningependa tu kuchukua hatua kulingana na nia Zako na kutimiza mapenzi Yako. Nitakunywa kutoka kwenye kikombe Chako kichungu, na mimi ni Wako wa kuamuru.”

Lazima muwe wazi kuhusu njia mnayotembelea; lazima muwe wazi kuhusu njia mtakayotumia kwenye siku za usoni, ni nini haswa ambacho Mungu atafanya kuwa timilifu na ni nini mlichoaminishiwa. Siku moja, pengine, utajaribiwa, na kama wakati huo mtaweza kupata mhemko kutoka kwa yale aliyopitia Petro, utawaonyesha kwamba kwa kweli unatembea njia ya Petro. Petro alipongezwa na Mungu kwa imani na upendo wake wa kweli, na kwa utiifu wake kwa Mungu. Na ilikuwa kutokana na uaminifu wake na kutamani kwake kwa Mungu katika moyo wake ndiposa Mungu akamfanya kuwa timilifu. Kama kweli unao upendo na imani kama hiyo ya Petro, basi Yesu kwa kweli atakufanya kuwa timilifu.

Tanbihi:

Maandishi ya asilia yanasoma “kwa maneno haya.”