Swahili

Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu

Kufahamu kazi ya Mungu, athari inayotimizwa kwa mwanadamu, na mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu, hiki ndicho kitu ambacho kila mtu anayemfuata Mungu anapaswa kutimiza. Sasa wanachokosa watu wote ni ufahamu wa kazi ya Mungu. Mwanadamu haelewi wala kufahamu kabisa maana ya vitendo vya Mungu ndani ya mwanadamu, kazi yote ya Mungu, na mapenzi ya Mungu tangu kuumbwa kwa dunia. Huu upungufu hauonekani tu katika ulimwengu mzima wa kidini, lakini zaidi ya hayo kwa waumini wote wa Mungu. Siku itakapofika utakapomtazama Mungu kwa kweli na kutambua hekima ya Mungu; utakapotazama matendo yote ya Mungu na kutambua kile Mungu Alicho na kile Alicho nacho; utakapotazama wingi Wake, hekima, ajabu Yake, na kazi Yake yote kwa mwanadamu, basi hapo ndipo utakuwa umefikia imani ya mafanikio kwa Mungu. Mungu anaposemekana kuwa anajumuisha yote na tele zaidi, ni nini kinachomaanishwa na kujumuisha yote? Na nini kinachomaanishwa na tele? Iwapo huelewi haya, basi huwezi kuchukuliwa kuwa muumini wa Mungu. Mbona Nasema wale walio katika dunia ya kidini hawaamini katika Mungu na ni waovu, walio sawa na ibilisi? Ninaposema ni watenda maovu, ni kwa sababu hawaelewi matakwa ya Mungu, wala kuona hekima Yake. Hakuna wakati ambao Mungu anadhihirisha kazi Yake kwao; ni vipofu, wasioona matendo ya Mungu. Wao ndio walioachwa na Mungu na hawamiliki kabisa utunzaji na ulinzi wa Mungu, sembuse kazi ya Roho Mtakatifu. Wale walio bila kazi ya Mungu ni watenda maovu na humpinga Mungu. Wale Ninaosema wanampinga Mungu ni wale wasiomjua Mungu, wale wanaokiri Mungu na maneno matupu ilhali hawamjui, wale wanaomfuata Mungu lakini hawamtii, na wale wanaofurahia neema ya Mungu lakini hawawezi kumshuhudia. Bila ufahamu wa madhumuni ya kazi ya Mungu na kazi ya Mungu kwa mwanadamu, mwanadamu hawezi kuwa katika ulinganifu na moyo wa Mungu, na hawezi kumshuhudia Mungu. Sababu kwamba mwanadamu humpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wanafunzi katika imani wanampinga Mungu kwa sababu upinzani kama huu uko ndani ya asili yao, ilhali upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomfahamu Mungu, kuongeza kwa tabia yao potovu. Kwa muda kabla ya Mungu kuwa mwili, kipimo cha kama mwanadamu alimpinga Mungu kilikuwa iwapo alihifadhi amri zilizotolewa na Mungu mbinguni. Kwa mfano, katika Enzi ya Sheria, wowote ambao hawakuhifadhi sheria za Yehova walikuwa ndio wale waliompinga Mungu; wowote walioiba sadaka ya Yehova, na wowote waliosimama dhidi ya wale waliofadhiliwa na Yehova walikuwa wale waliompinga Mungu na wale ambao wangepigwa mawe hadi kufa; wowote ambao hawakuheshimu mama na baba zao, na wowote waliompiga ama kumlaani mwingine ni wale ambao hawakufuata sheria. Na wote ambao hawakufuata sheria za Yehova walikuwa wale waliosimama dhidi Yake. Hii haikuwa hivyo tena katika Enzi ya Neema, wakati wale waliosimama dhidi ya Yesu walikuwa wale waliosimama dhidi ya Mungu, na wowote ambao hawakutii maneno yaliyotamka na Yesu ni wale waliosimama dhidi ya Mungu. Katika enzi hii, makusudio ya “upinzani kwa Mungu” yalifafanuliwa zaidi na kuwa halisi. Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa “upinzani kwa Mungu” wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vile mwanadamu alivyomwamini Mungu katika mawazo yake, Mungu hakumlaumu mwanadamu ama kuulizia mengi kutoka kwa mwanadamu, kwani mwanadamu hangemwona Mungu hata kidogo. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo vya Mungu katika mwili. Wakati huo, dhana zote za mwanadamu zinafutwa na kubaki povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi. Wale walio na dhana kumhusu Mungu lakini bado wanatii kwa furaha hawatalaaniwa. Mungu anamlaani mwanadamu kulingana na nia yake na vitendo vyake, kamwe sio kwa mawazo na fikira zake. Iwapo mwanadamu angelaaniwa kwa misingi hiyo, basi hakuna mmoja ambaye angeweza kutoroka kutoka katika mikono ya Mungu ya ghadhabu. Wanaosimama makusudi dhidi ya Mungu mwenye mwili wataadhibiwa kwa sababu ya kutotii kwao. Upinzani wao wa makusudi unatokana na dhana zao kumhusu, ambao unasababisha usumbufu wao kwa kazi ya Mungu. Wanadamu kama hao wanapinga na kuiharibu kazi ya Mungu wakijua. Hawana tu dhana za Mungu, lakini wanafanya kile kinachosumbua kazi Yake, na ni kwa sababu hii ndio wanadamu kama hao watahukumiwa. Wale wasioshiriki katika usumbufu wa kazi kimakusudi huwahukumiwa kama wenye dhambi, kwani wanaweza kutii kwa makusudi na kutosababisha vurugu na usumbufu. Wanadamu kama hao hawatahukumiwa. Hata hivyo, wakati wanadamu wamepata uzoefu wa miaka mingi ya kazi ya Mungu, kama bado wanaficha dhana zao za Mungu na kubaki wasioweza kujua kazi ya Mungu mwenye mwili, na licha ya miaka mingi ya uzoefu, wanaendelea kushikilia dhana nyingi za Mungu na hawawezi bado kuja kumjua Mungu, basi hata kama hawasababishi shida yoyote kukiwa na dhana nyingi za Mungu ndani ya mioyo yao, na hata kama dhana kama hizi hazionekani, wanadamu kama hao hawana huduma yoyote kwa kazi ya Mungu. Hawawezi kuhubiri injili wala kumshuhudia Mungu; wanadamu kama hao hawana manufaa na ni wapumbavu. Kwa sababu hawamjui Mungu na hawawezi kuondoa dhana zao za Mungu, wamelaaniwa. Inaweza kusemwa hivi: Ni kawaida kwa wanafunzi wa kidini kuwa na dhana za Mungu ama kutojua chochote kumhusu, lakini sio kawaida kwa wale walioamini kwa miaka mingi na kuwa na uzoefu mwingi wa kazi Yake kushikilia dhana kama hizi, na hata zaidi kwa wanadamu kama hao kutokuwa na ufahamu wa Mungu. Ni kwa sababu ya hali kama hii isiyo ya kawaida ndio wanadamu kama hao wanalaaniwa. Wanadamu wasio wa kawaida kama hao hawana manufaa; ni wale wanaompinga Mungu zaidi na waliofurahia neema ya Mungu bure. Wanadamu wote kama hao wataondolewa mwishoni!

Wowote wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu ni wale wanaompinga Mungu, na hata zaidi ya hayo ni wale waliofahamu madhumuni ya kazi ya Mungu lakini bado hawatafuti kumridhisha Mungu. Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama kufundisha juu ya Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga makusudi. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, wakiongoza pepo zinazowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza? Wale wanaojiheshimu mbele ya Mungu ni wanadamu wa chini kabisa, ilhali wanaojinyenyekeza ndio wa heshima zaidi. Na wale wanaojifikiria kujua kazi ya Mungu na kutangaza neno la Mungu kwa wengine kwa mshindo wa tarumbeta nyingi wakati macho yao yako Kwake—hawa ndio wajinga zaidi kati ya wanadamu. Wanadamu kama hao ni wale wasio na ushahidi wa Mungu, na wale walio na kiburi na majivuno. Wale wanaoamini kwamba wana ufahamu mdogo wa Mungu licha ya uzoefu wao halisi na ufahamu wa vitendo ni wale Anaowapenda zaidi. Ni wanadamu kama hawa ndio walio na ushahidi wa kweli na wanaweza kweli kukamilishwa na Mungu. Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya dutu ya maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli mna imani ya kutembea njia hii, basi zidini kuifuata. Iwapo hamwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kuenda zenu kabla hamjachelewa.Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Hamna uaminifu ama utii hata kidogo, ama mioyo ilio na kiu ya haki na ukweli. Na wala hamna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yenu mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Hamwezi kuweka mnachopaswa wala kusema mnachopaswa. Hamwezi kuweka katika vitendo kile ambacho mnapaswa, na hamwezi kufanya kazi mnayopaswa. Hamna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio mnalopasa. Hamjavumilia mateso mnayopaswa kuwa mmevumilia, na hamna imani mnayopaswa kuwa nayo. Hamna sifa yoyote kabisa; mna heshima binafsi ya kuendelea kuishi? Nawahimiza kwamba mko bora kufunga macho kwa mapumziko ya milele, hivyo kumtoa Mungu katika kujishughulisha nanyi na kuvumilia mateso kwa ajili yenu. Mnaamini katika Mungu lakini bado hamjui mapenzi Yake; mnakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado hamwezi kukidhi mahitaji Yake. Mnaamini katika Mungu lakini bado hamumjui, na kuishi ingawa hamna lengo la kujaribu kufikia. Hamna maadili na hamna madhumuni. Mnaishi kama wanadamu lakini hamna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Mnafikiriwaje kuwa wanadamu? Mnaamini katika Mungu lakini mnamdanganya. Juu ya hayo, mnachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, hamwonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Hamwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu yasiyo ya maana. Kwa hivyo mnawezaje kufikiriwa kuwa wanadamu? Chakula mnachokula na hewa mnayopumua vimetoka kwa Mungu, mnafurahia neema Yake, na bado mwishowe, hamna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, mmekuwa watu wasio na maana wanaompinga Mungu. Si basi nyinyi ni wanyama wasio bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kuwaliko?

Hao wahubiri na wazee wanaosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu ni wapinzani wa Mungu na wako katika muungano na Shetani; wale kati yenu wasiosimama katika mimbari ya juu wakimfundisha mwanadamu hawatakuwa hata wapinzani wakubwa zaidi wa Mungu? Juu ya hayo, hamna ushirikiano basi na Shetani? Wale wasioelewa madhumuni ya kazi ya Mungu hawajui kuwa na makubaliano na moyo wa Mungu. Bila shaka, haiwezi kuwa ukweli kwa wale wanaoyaelewa madhumuni ya kazi Yake? Kazi ya Mungu kamwe haina makosa; badala yake, ni kufuatilia kwa mwanadamu kuliko na dosari. Wale wabaya wanaompinga Mungu makusudi sio waovu zaidi na mahasidi kuliko hao wahubiri na wazee? Wanaompinga Mungu ni wengi, na miongoni mwa wanadamu hao wengi, kuna aina mbalimbali ya upinzani dhidi ya Mungu. Kwa kuwa kuna kila aina ya waamini, hivyo pia kuna kila aina ya wale wanaompinga Mungu kila tofauti na kingine. Hakuna mmoja kati ya wale wasiotambua wazi madhumuni ya kazi ya Mungu anayeweza kuokolewa. Bila kujali jinsi mwanadamu anaweza kuwa alimpinga Mungu zamani, mwanadamu ajapo kufahamu madhumuni ya kazi ya Mungu na kujitolea juhudi zake ili kumridhisha Mungu, dhambi zake za awali zitafutiliwa mbali na Mungu. Bora tu mwanadamu anatafuta ukweli na kuuweka ukweli katika vitendo, Mungu hataweka akilini kile amefanya. Badala yake, ni kwa msingi wa kutenda ukweli kwa mwandamu ndiyo Mungu anamtetea mwanadamu. Hii ndiyo haki ya Mungu. Kabla ya mwanadamu kumwona Mungu ama kuwa na uzoefu wa kazi Yake, bila kujali jinsi mwanadamu anamtendea Mungu, Haliweki hili akilini. Hata hivyo, mara tu mwanadamu amwonapo Mungu, na kuwa na uzoefu wa kazi Yake, matendo yote na vitendo vyote vya mwanadamu vinaandikwa chini ndani ya “rekodi” na Mungu, kwani mwanadamu amemwona Mungu na kuishi ndani ya kazi Yake.

Wakati mwanadamu ameona kwa kweli kile Mungu alicho nacho na kile Alicho, aonapo ukuu Wake, na kweli kuja kujua kazi ya Mungu, na zaidi ya hayo, tabia ya awali ya mwanadamu inabadilika, basi mwanadamu atakuwa ameitupilia mbali kabisa tabia yake ya uasi inayompinga Mungu. Inaweza kusemwa kwamba kila mwanadamu amempinga Mungu wakati mmoja na kila mwanadamu ameasi dhidi ya Mungu. Hata hivyo, kama unamtii Mungu mwenye mwili kwa makusudi, na kwa hivyo kuuridhisha moyo wa Mungu kwa uaminifu wako, unaweka katika vitendo ukweli unaopaswa, kutekeleza jukumu lako unavyopaswa, na kufuata kanuni unavyopaswa, basi wewe ni mmoja aliye tayari kutupilia mbali uasi wake kumridhisha Mungu na mmoja anayeweza kukamilishwa na Mungu. Iwapo utakataa kutambua makosa yako na huna moyo wa kutubu; ukiendelea katika njia yako ya uasi na huna kabisa moyo wa kufanya kazi na Mungu na kumridhisha Mungu, basi mjinga mkaidi kama wewe kwa hakika ataadhibiwa na hatawahi kuwa mmoja wa kukamilishwa na Mungu. Iwapo hivyo, wewe ni adui wa Mungu leo na kesho, na hivyo pia utabaki adui wa Mungu siku ifuatayo; utakuwa milele mpinzani wa Mungu na adui wa Mungu. Mungu atakuachaje? Ni asili ya mwanadamu kumpinga Mungu, lakini mwanadamu hawezi kwa makusudi kutafuta “siri” za kumpinga Mungu kwa sababu kubadili asili yake ni kazi isiyoshindika. Kama hali ni hiyo, basi ni bora uende zako kabla hujachelewa, isiwe kurudi kwako wakati ujao kukawa kali zaidi, na isiwe asili yako kama ya mnyama ikaibuka na kuwa isiyotawalika mpaka mwili wako unaondolewa na Mungu mwishowe. Unaamini katika Mungu ili ubarikiwe; ikiwa mwishowe, balaa tu ndiyo itakayokupata, hiyo haitakuwa na thamani. Nawahimiza kuunda mpango mwingine; zoezi jingine litakuwa bora kuliko imani yenu kwa Mungu. Hakika kuna mengi kuliko njia hii moja? Hamngeweza kuendelea kuishi vile vile bila kutafuta ukweli? Mbona kuishi katika kutopatana na Mungu kwa namna hii?