Swahili

Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini

Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi wewe umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako mwenyewe? Ni mara ngapi wewe umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu wewe kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, haya ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Kutenda kama huku pekee ndiko hutosheleza Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli.

Baadhi ya watu wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya kaka na dada zake katika Kristo, anasema yeye ni mdeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, yeye hatii katika vitendo ukweli ila anafanya tofauti kabisa. Je, hii si ni kama wale Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya kufichua kwa nje. Yeye yuko tayari kutia katika vitendo ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali mazingira. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna baadhi ya watu ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kukaa katika hali isiyo halisi, na kuvalia uso bandia wa mnyonge. Aibu gani hii! Na kama ungemuuliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kuhusu uaminifu wako kwa umma, bali tumia matendo yako halisi ili kuonyesha upendo wako kwa Mungu, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wanasali, hata bila uwepo wa Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na mila na desturi za kidini na fikra; wanaishi na mila hizo na fikra kama hizo, daima wakiamini kwamba hatua kama hiyo humpendeza Mungu, na kwamba kumfuata Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo humpendeza Mungu. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanazungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa maksudi hujitoa wakati wowote kwa utumishi mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni namna ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana tabia za kiajabu na heshima, na anaweza kuwa shahidi kokote aendako; yeye ni mmoja wa wapenzi wa Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunja. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Namna hii ya watu ni watu wa dini, na ni wanafiki mno.

Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanaulizana, “Dada, uko vipi siku hizi?” Anajibu, “Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kutosheleza matakwa ya moyo Wake.” Mwengine anasema, “Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kukidhi matakwa Yake.” Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inaleta upinzani kwa Mungu. Wale ambao huzingatia ukweli halisi huwasilisha vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwenziwe anaimba, yeye anaanza kucheza, bila hata kujua kuwa wali kwenye sufuria yake umeshaungua. Watu wa namna hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni dalili za ukosefu wa ukweli! Baadhi yao hukusanyika kuzungumza kuhusu mambo ya maisha katika roho, na ingawa hawasemi kuhusu kuwa kwao wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani ya wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika hali halisi, si kwa bidii ya nje au maonyesho.

Je, matendo ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza tamaa za Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyakidhi maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo hamu ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, inawezekana kuwa unayoyataka wewe yanaweza kuwakilisha Anayotaka Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama wewe unahisi kuwa u mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuyazungumzia mambo haya kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unavuta nadhari kwako wewe mwenyewe mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza hamu ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima ni katika kuonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mema ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Wafarisayo wanafiki na watu wa dini! Msipoacha matendo yenu ya nje na hamuwezi kufanya mabadiliko, basi mambo ya unafiki ndani yenu yatazidi kuimarika. Namna mambo ya unafiki yanavyozidi kuwa, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, aina hii ya watu hakika watatupiliwa mbali!