Swahili

Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo ni Mungu Mwenyewe

Je, unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Mungu wa vitendo Mwenyewe anajumuisha Roho, Nafsi, na Neno, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa utendaji Mwenyewe. Kama unajua Nafsi pekee—kama unajua tabia na utu Wake—lakini hujui kazi ya Roho, au ambacho Roho hufanya katika mwili, na kuangazia Roho tu, na Neno, na kuomba mbele ya Roho, bila kujua kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hii inadhihirisha kuwa humjui Mungu wa vitendo. Ufahamu wa Mungu wa vitendo unajumuisha kujua na kuyapitia maneno Yake, na kuelewa sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Kwa hivyo, pia, inajumuisha kujua kwamba kila tendo la Mungu katika mwili linaongozwa na Roho, na kwamba maneno Anenayo ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ukitaka kumjua Mungu wa vitendo, lazima kimsingi ujue jinsi ambavyo Mungu hufanya kazi miongoni mwa wanadamu na katika uungu; hili, wakati ule ule, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote hujihusisha nayo.

Ni nini kilichomo katika maonyesho ya Roho? Wakati mwingine Mungu wa vitendo hufanya kazi miongoni mwa ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini kwa jumla, Roho anatawala katika pande zote mbili. Hata iwe ni roho gani ndani ya watu, hivyo ndivyo huwa maonyesho yao ya nje. Roho anafanya kazi kawaida, lakini kuna pande mbili za uelekezaji Wake kwa Roho: Upande mmoja ni kazi Yake kwa ubinadamu, na upande mwingine ni kupitia uungu. Unafaa kujua haya wazi wazi. Kazi ya Roho hubadilika kulingana na matukio: Wakati kazi Yake ya binadamu inahitajika, Roho anaielekeza kazi hii ya binadamu, na wakati kazi ya uungu inahitajika, uungu hujitokeza moja kwa moja kuifanya. Kwa sababu Mungu hufanya kazi katika mwili na kujionyesha katika mwili, Anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu. Kazi Yake katika ubinadamu inaongozwa na Roho, na ili kuyaridhisha mahitaji ya kimwili ya watu, kuwezesha ushirikiano wao Naye, kuwafanya waone uhalisi na ukawaida wa Mungu, na kuwafanya waone kuwa Roho amekuja katika Mwili, na Yuko miongoni mwa wanadamu, Anaishi pamoja na wanadamu, na Hushirikiana na wanadamu. Kazi Yake ya uungu ni kwa ajili ya kuwapa watu uzima, na kuwaelekeza watu katika kila kitu kwa upande mzuri, na kubadili tabia za watu na kuwafanya waone kwa kweli kuonekana kwa Roho katika mwili. Kwa kiwango kikubwa, ukuaji katika maisha ya mwanadamu unapatikana moja kwa moja kupitia kazi ya Mungu na maneno katika uungu. Ikiwa tu watu wataikubali kazi ya Mungu ya uungu wataweza kubadili tabia zao, hapo tu ndipo wataweza kushibishwa katika roho zao; ikiwa tu kuna ongezeko la kazi kwa ubinadamu katika mambo hayo—uchungaji wa Mungu, usaidizi, na riziki kwa ubinadamu—ndipo watu wataweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Kama watakaa kulingana na amri, angalau watu wanapaswa kumjua Mungu wa vitendo anayeonekana kwa mwili, bila kuchanganyikiwa. Kwa maneno mengine, watu wanapaswa kufahamu kanuni za kuzifuata amri. Kufuata amri hakumaanishi kuzifuata ovyo ovyo au kiholela, bali kuzifuata kwa msingi, na lengo, na kanuni. Kitu cha kwanza kufanikishwa ni kwamba maono yako yawe wazi. Mungu wa vitendo Mwenyewe ambaye Anazungumziwa leo hufanya Kazi katika uungu na ubinadamu. Kupitia kwa kujitokeza kwa Mungu wa vitendo, kazi Yake ya kawaida ya binadamu na maisha na kazi Yake kamilifu ya uungu vinapatikana. Ubinadamu na uungu wake vimeungwa kuwa kitu kimoja, na kazi ya pande zote mbili inakamilishwa[a] kupitia maneno; iwe katika ubinadamu au uungu, Ananena maneno. Mungu anapofanya Kazi katika ubinadamu, Anazungumza lugha ya ubinadamu, ili watu waweze kushiriki na kuelewa. Maneno Yake yanasemwa waziwazi, na ni rahisi kueleweka, kiasi kwamba yanaweza kutolewa kwa watu wote; bila ya kujali kuwa hawa watu wana ufahamu au hawajasoma vyema, wote wanaweza kupokea maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu katika uungu vilevile inaweza kufanywa kupitia maneno, lakini imejawa na riziki, imejawa na uzima, haijatiwa dosari na mawazo ya mwanadamu, haihusishi mapenzi ya mwanadamu, na haina mipaka ya binadamu, iko nje ya mipaka ya ubinadamu wowote wa kawaida; vilevile, inafanywa katika mwili, lakini ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Kama watu wanaikubali kazi ya Mungu katika ubinadamu tu, basi watajiwekea mipaka katika upeo fulani, na hivyo milele watahitaji kushughulikiwa, kupogolewa, na kufundishwa nidhamu ili kwamba pawepo na mabadiliko kidogo ndani yao. Bila ya Kazi au uwepo wa Roho Mtakatifu, ingawa, watairudia mienendo yao ya awali; ni kupitia kazi ya uungu tu ndio haya maradhi na upungufu vitaweza kurekebishwa, hapo ndipo watu wanafanywa kuwa wakamilifu. Badala ya kushughulikia na kupogoa mara kwa mara, kinachohitajika ni matokeo mazuri, kwa kutumia maneno kufidia upungufu wote, kutumia maneno ili kufichua hali zote za watu, kutumia maneno kuyaelekeza maisha yao, kila matamshi yao, kila tendo lao, ili kuziweka wazi nia na motisha yao; hii ni kazi halisi ya Mungu wa vitendo. Na kwa hivyo, katika mwelekeo wako kwa Mungu wa vitendo unafaa kunyenyekea mbele ya ubinadamu Wake, ukimkubali na kumtambua, na zaidi, unapaswa kukubali na kutii kazi ya uungu na maneno. Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kuwa kazi yote na maneno ya Roho wa Mungu yanafanywa katika ubinadamu wake wa kawaida, na kupitia mwili Wake uliopatikana. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu huelekeza kazi Yake ya ubinadamu na hutekeleza kazi Yake ya uungu katika mwili, na katika Mungu kupata mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi kamili ya uungu; huu ndio umuhimu hasa wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ukiweza kuliona hili wazi, utaweza kuhusisha sehemu zote za Mungu, na utaacha kuthamini sana kazi Yake ya uungu, na kuwa mwenye kupuuza sana kazi Yake katika ubinadamu, na hautazidi mipaka wala kupita njia za michepuo. Kwa jumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kuwa kazi Yake ya ubinadamu na kazi Yake ya uungu, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waone kuwa Yeye ni wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, na ni halisi na wa hakika.

Roho wa kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu ana awamu za mpito. Kwa kuwafanya wanadamu wakamilifu, Anawawezesha wanadamu Wake kupokea mwelekeo wa Roho, baadaye Wanadamu Wake wanaweza kuanzisha na kuyaongoza makanisa. Hii ni aina moja ya maonyesho ya kazi ya kawaida ya Mungu. Hivyo, ukiweza kuona wazi kanuni za kazi ya Mungu kwa wanadamu, basi itakuwa vigumu kwako kuwa na dhana kuhusu kazi ya Mungu kwa wanadamu. Bila kujali kitu kingine chochote, Roho wa Mungu hawezi kukosea. Yuko sahihi, na Hana dosari; Hawezi kufanya kitu chochote kimakosa. Kazi ya uungu ni maonyesho ya moja kwa moja ya mapenzi ya Mungu, bila maingilio ya mwanadamu. Haipitii ukamilifu, ila inatoka moja kwa moja kwa Roho. Na bado, kufanya Kwake kazi katika uungu ni kwa sababu ya ubinadamu Wake wa kawaida; si miujiza, na kazi inaonekana kana kwamba imefanywa na mwanadamu wa kawaida; Kimsingi Mungu alitoka mbinguni kuja duniani ili kuonyesha maneno ya Mungu kupitia mwili, kukamilisha kazi ya Roho wa Mungu kwa kutumia mwili.

Ufahamu wa watu leo kuhusu Mungu wa vitendo bado unaegemea upande mmoja, na ufahamu wao kuhusu umuhimu wa kupata mwili ni mdogo sana. Kuhusu suala la mwili wa Mungu, kupitia kwa kazi na maneno Yake watu huona kuwa Roho wa Mungu ana mengi, kwamba ni tajiri. Lakini, hata hivyo, ushuhuda wa Mungu hatimaye hutoka kwa Roho wa Mungu: Anachokifanya Mungu katika Mwili, ni kanuni gani anatumia, anachokifanya katika ubinadamu, na anachokifanya katika uungu. Leo unaweza kumwabudu huyu mtu, lakini kwa hakika unamwabudu Roho. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa kinachopaswa kufahamiwa kuhusu ufahamu wa watu kuhusu Mungu aliyepata mwili: kujua kiini cha Roho kupitia kwa mwili, kujua kazi ya uungu ya Roho katika mwili na kazi ya wanadamu katika mwili, kukubali maneno yote ya Roho na matamshi katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anauelekeza mwili na kudhihirisha uwezo Wake katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, mwanadamu anapata kumjua Roho aliye mbinguni kupitia kwa mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumemwondoa Mungu asiye yakini kutoka katika dhana za wanadamu; ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utiifu wao kwa Mungu; na kupitia kwa uungu wa kazi ya Roho wa Mungu katika Mwili, na kazi ya wanadamu katika miili, mwanadamu hupata ufunuo, na kuongozwa, na mabadiliko hupatikana katika tabia ya maisha yake. Hii tu ndiyo maana halisi ya ujio wa Roho katika mwili, kimsingi, ili kwamba watu waweze kushirikiana na Mungu, kumtegemea Mungu, na kuupata ufahamu wa Mungu.

Kwa kiasi kikubwa, ni mtazamo upi watu wanapaswa kuwa nao kuhusu Mungu wa vitendo? Unajua nini kuhusu kupata mwili, kuhusu kuonekana kwa Neno katika mwili, kuhusu kuonekana kwa Mungu katika mwili, na matendo ya Mungu wa vitendo? Na nini inazungumzia zaidi leo? Kupata mwili, ujio wa Neno katika mwili, kuonekana kwa Mungu katika mwili—haya yote ni lazima yaeleweke. Kwa kuzingatia kimo chenu, na enzi, ni lazima mpate kuyaelewa haya masuala hatua kwa hatua, katika uzoefu wa maisha yenu, ni lazima mpate kuyaelewa haya masuala hatua kwa hatua, na ni lazima muwe na ufahamu ulio wazi. Mchakato ambamo watu huyapitia maneno ya Mungu ni sawa na mchakato ambamo wanafahamu kujitokeza kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyoyapitia maneno ya Mungu, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu; kwa kuyapitia maneno ya Mungu, watu wanaelewa kanuni za kazi ya Roho na kupata kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa hakika, Mungu akiwafanya watu wakamilifu na kuwachukua, Anawafanya wayajue matendo ya Mungu wa vitendo; Anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, na kuwaonyesha kuwa Roho wa Mungu hakika ameonekana kwa mwanadamu. Watu wakichukuliwa na kufanywa wakamilifu na Mungu, maonyesho ya Mungu wa vitendo huwa amewashinda, maneno ya Mungu wa vitendo huwa yamewabadilisha, na kutoa uzima Wake ndani yao, kuwajaza na kile Alicho (iwe ni uwepo wake wa binadamu, au ule wa uungu), kuwajaza kwa kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu akiwapata watu, kimsingi Anafanya hivyo kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo ili kuushughulikia upungufu wa watu, na kuhukumu na kufichua tabia zao za uasi, kuwafanya wapate wanachokihitaji, na kuwaonyesha kuwa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi, kazi ifanywayo na Mungu wa vitendo ni kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa katika nchi ya uchafu, na kuziondoa tabia zao potovu. Umuhimu mkubwa zaidi wa watu kupatikana na Mungu wa vitendo ni kuwa na uwezo wa kumfanya Mungu wa vitendo kielelezo, na kuishi kulingana na ubinadamu wa kawaida, kuweza kutenda kulingana na maneno na mahitaji ya Mungu wa vitendo, bila upotofu au kuteleza, kutenda kama Asemavyo, na kuweza kufanikisha lolote Atakalo. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu. Ukipatwa na Mungu, hupati tu kazi ya Roho Mtakatifu; kidesturi, unaweza kuzidisha mahitaji ya Mungu wa utendaji. Kuwa tu na kazi ya Roho Mtakatifu hakumaanishi kuwa una uzima. Cha muhimu ni kama unaweza kuishi kwa kudhihirisha mahitaji ya Mungu wa vitendo, ambayo inahusiana na kama unaweza kupatikana na Mungu. Haya mambo ndiyo muhimu zaidi katika kazi ya Mungu wa vitendo katika mwili. Hivi ni kusema kuwa, Mungu analipata kundi la watu kwa kuonekana halisi na hakika katika mwili na kuwa wazi na mwenye kufanana na kiumbe chenye uhai, Akionekana na watu, hasa Akifanya kazi ya Roho katika mwili, na kwa kuwa kielelezo kwa watu wenye miili. Kimsingi, ujio wa Mungu katika mwili ni kuwawezesha watu kuona matendo halisi ya Mungu, kumfanya Roho asiye na umbo kuwa bayana katika mwili, na kuwapa watu fursa ya kumwona na kumgusa. Kwa njia hii, wanaokamilishwa Naye wataishi kwa kumfuata Yeye, watamfaidi na kuupendeza moyo Wake. Mungu angalinena kutoka mbinguni tu, na hakika asije duniani, basi bado watu hawangeweza kumjua, wangeweza tu kuyahubiri matendo ya Mungu kwa kutumia nadharia tupu, na hawangekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Mungu amekuja duniani kimsingi kuwa mfano na kielelezo kwa wale ambao wamepatwa na Mungu; ni kwa njia hii pekee ndio watu wanaweza kumjua Mungu kwa hakika, na kumgusa Mungu, na kumwona, na hapo ndipo wanaweza kupatikana na Mungu kwa kweli.

Tanbihi:

a. Matini asilia inasomeka “na zote mbili ni.”