Swahili

Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha awamu tatu, au enzi tatu: Kwanza, Enzi ya Sheria; pili, Enzi ya Neema (ambayo pia ni enzi ya Ukombozi); na mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, sahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani anatumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kutoa wazi hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake. Ni kuonyesha hekima Yangu na kudura na wakati uo huo kufunua ubovu wa Shetani. Aidha, ni kufundisha viumbe Wangu kubagua kati ya mema na mabaya, kutambua kwamba Mimi ndiye Mtawala wa vitu vyote, kuona wazi kwamba Shetani ni adui wa binadamu, wa chini kuliko wote, yule mwovu, na kufanya tofauti kati ya mema na mabaya, ukweli na uwongo, utakatifu na uchafu, ukuu na udogo, wazi kama mchana. Kwa njia hii, binadamu wasiofahamu wanaweza kunishuhudia kwamba si Mimi Ninayewapotosha wanadamu, na kwamba ni Mimi tu—Muumba—Ninayeweza kumwokoa binadamu, Naweza kuwapa mambo kwa ajili ya raha; na wapate kujua kwamba Mimi Ndimi Mtawala wa vitu vyote na kwamba Shetani ni mmoja tu wa viumbe Vyangu, ambaye baadaye alinigeuka. Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita umegawanywa katika hatua tatu ili kufikia matokeo yafuatayo: Kuruhusu viumbe Wangu wawe mashahidi Wangu, kujua mapenzi Yangu, na waone kwamba Mimi Ndimi ukweli. Hivyo, wakati wa kazi ya mwanzo wa Mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, Nilifanya kazi ya sheria, ambayo ilikuwa ni kazi ya Yehova kuwaongoza watu. Hatua ya pili ilikuwa kuanza kazi ya Enzi ya Neema katika vijiji vya Yudea. Yesu Anawakilisha kazi yote ya Enzi ya Neema; Alikuwa mwili na kusulubiwa, na Akazindua Enzi ya Neema. Alisulubiwa ili kukamilisha kazi ya ukombozi, ili kumaliza Enzi ya Sheria na kuanzisha Enzi ya Neema, na hivyo Yeye Aliitwa “Kamanda Mkuu”, “Sadaka ya Dhambi,” “Mkombozi.” Kwa hiyo kazi ya Yesu ilitofautiana katika maudhui kutokana na kazi ya Yehova, ingawa zilikuwa sawa katika kanuni. Yehova Alianzisha Enzi ya Sheria, Akajenga msingi imara wa nyumbani, mahali pa kuzaliwa pa kazi Yake hapa duniani, na Alitoa amri; haya yalikuwa mafanikio Yake mawili, yanayowakilisha Enzi ya Sheria. Kazi ya Yesu haikuwa kutoa amri, bali kutimiza amri, na hivyo kutangaza Enzi ya Neema na kuhitimisha Enzi ya Sheria ambayo ilidumu kwa miaka elfu mbili. Alikuwa mwanzilishi, kuikaribisha Enzi ya Neema, ilhali ukombozi ulibakia msingi wa kazi Yake. Na hivyo mafanikio Yake Yalikuwa pia mara mbili: kufungua enzi mpya, na kukamilisha kazi ya ukombozi kupitia kusulubiwa Kwake. Kisha Akaondoka. Katika hatua hiyo, Enzi ya Sheria ilifikia mwisho wake na mwanadamu aliingia katika Enzi ya Neema.

Kazi ya Yesu ilifanyika kulingana na mahitaji ya mwanadamu katika enzi hiyo. Kazi Yake ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu, kuwasamehe dhambi zao, na kwa hivyo tabia Yake yote ilikuwa ya unyenyekevu, uvumilivu, upendo, ucha Mungu, uvumilivu, huruma na fadhili. Alibariki binadamu maradufu na kuwaletea neema kwa wingi, na mambo yote ambayo wangeweza kufurahia, Aliwapa kwa ajili ya furaha yao: amani na furaha, uvumilivu wa Yesu na upendo, huruma Yake na fadhili. Katika siku hizo, alichokutana nacho mwanadamu kilikuwa wingi wa vitu vya kufurahia tu: Moyo wake ulikuwa na amani na uhakikisho, Roho yake ilifarijika, na alikuwa anaendelezwa na Mwokozi Yesu. Sababu iliyomfanya mwanadamu aweze kufaidi mambo haya ni matokeo ya enzi alimoishi. Katika Enzi ya Neema mwanadamu alikuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo kazi ya ukombozi wa wanadamu wote ulihitaji wingi wa neema, ustahimili usio na mwisho na uvumilivu, na hata zaidi, sadaka ya kutosha kulipia dhambi za wanadamu, ili kufikia athari yake. Kile wanadamu waliona katika Enzi ya Neema kilikuwa tu sadaka Yangu ya dhambi ya binadamu, Yesu. Na walijua kwamba ni Mungu tu ndiye Anaweza kuwa mwenye huruma na uvumilivu, na waliona tu huruma wa Yesu na fadhili Zake. Hii ni kwa sababu wao waliishi katika Enzi ya Neema. Hivyo kabla ya kukombolewa, walilazimika kufurahia neema nyingi ambayo Yesu aliwapa; hili pekee ndilo lilikuwa la manufaa kwao. Kwa njia hii, wangeweza kusamehewa dhambi zao kupitia kufurahia kwao neema, na wangeweza kuwa na nafasi ya kukombolewa kupitia kufurahia kwa ustahimili wa Yesu na uvumilivu. Ni kwa njia ya ustahimili wa Yesu na uvumilivu ndio walikuwa na uwezo wa kupokea msamaha na kufurahia wingi wa neema kutoka kwa Yesu-kama vile Yesu alisema, “Nimekuja si kuwakomboa watu watakatifu, ila wenye dhambi, ili dhambi zao zisamehewe.” Kama Yesu angekuwa mwili na tabia ya hukumu, laana, na kutovumilia makosa ya mwanadamu, basi mwanadamu kamwe hangeweza kupata nafasi ya kukombolewa, na daima yeye angebaki mwenye dhambi; na hivyo mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeendelea zaidi ya Enzi ya Sheria. Enzi ya Sheria ingeendelea kwa miaka elfu sita, dhambi za mwanadamu zingeongezeka zaidi katika idadi na ziwe mbaya zaidi, na uumbaji wa binadamu ungekuwa wa bure. Wanadamu wangeweza tu kumtumikia Yehova chini ya Sheria, bali dhambi zao zingezidi za wanadamu wa kwanza kuumbwa. Jinsi Yesu alivyompenda mwanadamu zaidi, kusamehe dhambi zao na kuwapa huruma ya kutosha na fadhili, ndivyo wanadamu walizidi kuwa na uwezo wa kuokolewa, na kuitwa wanakondoo waliopotea ambao Yesu Aliwanunua tena kwa thamani kubwa. Shetani hakuweza kuingilia katika kazi hii, kwa sababu Yesu Aliwatunza wafuasi Wake kama mama mwenye upendo anachunga watoto wachanga walio katika mikono yake. Yeye hakuwa na hasira kwao au kuwadharau, bali Alikuwa Amejaa faraja; Yeye kamwe hakuwa na hasira miongoni mwao, lakini alistahimili makosa yao na akageuza jicho la kipofu kwa upumbavu wao na kutofahamu, hata Alisema, “Uwasamehe wengine mara sabini mara saba.” Kwa hiyo moyo Wake ulirekebisha mioyo ya wengine, na kwa njia hii ndiyo watu walipokea msamaha kupitia uvumilivu Wake.

Licha ya Yesu, kwa kuwa Mungu mwenye mwili, na kuwa bila hisia kabisa, Yeye daima Aliwafariji wanafunzi Wake, Aliwapa mahitaji yao, Akawasaidia, na Akawaendeleza. Bila kujali kiwango cha kazi Aliyofanya au kiasi gani cha mateso Alivumilia, Yeye kamwe hakuwa na matarajio kupita kiasi kwa mwanadamu, lakini kila mara Alikuwa mwenye subira na kuvumilia dhambi zao, kiasi kwamba katika Enzi ya Neema Alijulikana kwa upendo kama “Mpendwa Mwokozi Yesu.” Kwa watu wa wakati huo-na kwa watu wote. Kile Yesu Alikuwa nacho na kile Alichokuwa, ilikuwa huruma na fadhili. Yeye kamwe hakukumbuka makosa ya watu au kuruhusu makosa yao kuathiri jinsi Yeye Alivyowachukulia. Kwa sababu hiyo ilikuwa enzi tofauti, mara nyingi Alitoa chakula na vinywaji kwa watu ili waweze kula wasiweze tena. Yeye Aliwatendea wafuasi Wake wote kwa ukarimu, kuponya wagonjwa, kufukuza mapepo na kufufua wafu. Ili kwamba watu waweze kumwamini na kuona kwamba yote Aliyofanya yalifanyika kwa bidii na kwa dhati, Yeye Alifanya mpaka kiwango cha kufufua maiti iliyooza, kuwaonyesha kwamba mikononi Mwake hata wafu wanaweza kuwa hai tena. Kwa njia hii Alivumilia kwa kimya kati yao na Alifanya kazi Yake ya ukombozi. Hata kabla Asulubiwe msalabani, Yesu Alikuwa tayari Amebeba dhambi za binadamu na kuwa sadaka ya dhambi kwa wanadamu. Alikuwa tayari Amefungua njia ya msalaba ili kumkomboa mwanadamu kabla hajasulubiwa. Mwishowe Aligongwa misumari msalabani, Alijitoa sadaka yeye mwenyewe kwa ajili ya msalaba, na Aliweka huruma Yake yote, fadhili Zake, na utakatifu juu ya mwanadamu. Aliendelea kuvumilia wanadamu, kamwe Hakutafuta kulipiza kisasi, lakini kuwasamehe hao dhambi zao, Akiwasihi watubu, na kuwafundisha kuwa na subira, uvumilivu na upendo, kufuata nyayo Zake na kujitoa wenyewe kwa ajili ya msalaba. Upendo wake kwa ndugu na dada uilizidi upendo wake kwa Maria. Kanuni ya kazi Aliyofanya ilikuwa kuwaponya watu na kutoa mapepo, yote kwa ajili ya ukombozi Wake. Haijalishi Alikoenda, Yeye Aliwachukua wote waliomfuata kwa wema. Aliwafanya maskini kuwa tajiri, viwete wakatembea, vipofu wakaona, viziwi wakasikia; Yeye Aliwaalika mpaka watu wasiofaa machoni pa wanadamu na maskini zaidi, wenye dhambi, wakala pamoja Naye, Hakuepukana nao ila daima Alikuwa na subira, hata Akasema, “Wakati mchungaji anapoteza kondoo mmoja kati ya mia, yeye huondoka na kuwaacha nyuma wale tisini na tisa ili amtafute kondoo mmoja aliyepotea, na anapompata yeye hufurahia kwa shangwe.” Yeye Aliwapenda wafuasi wake kama kondoo anavyopenda wanakondoo wake. Ingawa walikuwa wajinga na wasio na ufahamu, na wenye dhambi katika macho Yake, na zaidi walikuwa washirika wa chini zaidi katika jamii, Aliona hawa wenye dhambi—waliodharauliwa na wengine—kama vipenzi Vyake. Kwa kuwa Alikuwa na fadhila kwao, Alitoa uhai Wake kwa ajili yao, kama mwana kondoo aliyetolewa madhabahuni. Alitembea kati yao kama mtumishi wao, Akawaruhusu kumtumia na kumchinja, Alijiwasilisha kwao bila masharti. Kwa wafuasi Wake Alikuwa Mpendwa Mwokozi Yesu, lakini kwa Mafarisayo, ambao waliwahubiria watu kutoka viweko vya mnara, Hakuwaonyesha huruma na wema, bali Yeye Aliwachukia na kuchukizwa nao. Hakufanya kazi sana miongoni mwa Mafarisayo, mara chache tu Aliwahubiria na kuwakemea; Yeye hakuwakomboa, au kufanya ishara na miujiza kati yao. Alihifadhi huruma Yake na upendo kwa wafuasi Wake, kuvumilia kwa ajili ya hawa wenye dhambi mpaka mwisho wakati Alipigwa misumari msalabani, kustahimili kila udhalilishaji mpaka Alivyowakomboa wanadamu wote kikamilifu. Hii ndio ilikuwa jumla ya kazi Yake.

Bila ukombozi wa Yesu, wanadamu wangeishi milele katika dhambi, na kuwa watoto wa dhambi, kizazi cha mapepo. Kama ingeendelea hivyo, Shetani angechukua makazi duniani, na dunia nzima ingekuwa makao yake. Lakini kazi ya ukombozi ilihitaji huruma na fadhili kwa wanadamu; kupitia kwa kazi hiyo tu ndio mwanadamu angeweza kupokea msamaha na mwishowe afuzu kufanywa kuwa mkamilifu na kupatwa kikamilifu. Bila hatua hii ya kazi, mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita haungeweza kuendelea mbele. Kama Yesu hangesulubiwa, kama Yeye Angewaponya tu watu na kufukuza mapepo, basi watu hawangesamehewa dhambi zao kikamilifu. Miaka mitatu na nusu ambayo Yesu Alifanya kazi Yake hapa duniani ilikamilisha tu nusu ya kazi Yake ya ukombozi; kisha kwa kupigiliwa misumari msalabani na kuwa na mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kukabidhiwa kwa mwovu, Yeye Alikamilisha kazi ya kusulubiwa na Akaanzisha hatima ya mwanadamu. Baada ya Yesu kukabidhiwa mikononi mwa Shetani tu, ndipo mwanadamu alikombolewa. Kwa miaka thelathini na mitatu na nusu Aliteseka duniani, Alidhihakiwa, Akatukanwa, na Akaachwa pweke, Aliachwa hata bila mahali pa kulaza kichwa chake, Hakuwa hata na mahali pa kupumzika; kisha Akasulubiwa, nafsi Yake yote—mwili safi na usio na hatia—kupigiliwa misumari msalabani, na kupitia kila namna ya mateso. Wale waliokuwa madarakani wakamdhihaki na kumcharaza mijeledi, na askari hata wakamtemea mate usoni; ila Alibaki kimya na kuvumilia mpaka mwisho, Akinyenyekea na kujitoa bila masharti mpaka wakati wa kifo, ambapo Yeye Alikomboa binadamu wote. Hapo tu ndipo Aliruhusiwa kupumzika. Kazi ya Yesu inawakilisha tu Enzi ya Neema; haiwakilishi Enzi ya Sheria na si mbadala wa kazi ya siku za mwisho. Hiki ndicho kiini cha kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema, enzi ya pili ambayo binadamu amepitia—Enzi ya Ukombozi.